HabariPilipili FmPilipili FM News

Onyang’nyong’ ya Vamia Wakaazi Wa Changamwe

Wakaazi wa changamwe wanataka hatua za dharura zichukuliwe ili kudhibiti maradhi ya onyang’nyong’ ambayo yanahataraisha maisha ya wakazi wengi eneo hilo.

Wakizunguumza na meza yetu ya habari wakaazi Hao wameeleza kushangazwa na mkurupuko wa maradhi hayo ambayo tiba yake bado haijatambulika, wakisema yanadalili za kupoozesha viungo vya mwili.

Nao wahudumu wa boda boda boda wanasema  visa vya kuwabeba wagonjwa eneo hilo kuwapeleka hospitalini vimekuwa vya kuogofya kwani wanahofia kuambukizwa wakiwa kazini

Ugonjwa huu umetajwa kusababishwa na mbu wa mchana wengi wakimtaja mbu huyo kuwa wa rangi ya kijani na ambaye anaweza hata kumlemaza binadamu pale hatua za dharura zinapokosa kuchukuliwa.

 

Show More

Related Articles