HabariMilele FmSwahili

Zaidi ya wanafunzi elfu 1 kufadhiliwa masomo ya upili na ya vyuo vikuu kupitia mradi wa Wings To Fly

Zaidi ya wanafunzi elfu 1 wanatarajiwa kunufaika mwaka huu na mradi wa kufadhiliwa masomo ya upili na vyuo vikuu kupitia mpango wa Wings to Fly chini ya benki ya Equity. Afisa mkuu mtendaji James Mwangi anasema walipokea maombi kutoka kwa zaidi ya wanafunzi elfu 30 kote nchini. Anasema mpango utaendelea kuwafaidi wanafunzi wasiojiweza kujilipia karo kufadhili masomo yao. Jumla ya wanafunzi 100 waliopata alama ya A- katika matokeo ya KCSE mwaka jana ni miongoni mwa watakaonufaika na mpango huo

Show More

Related Articles