HabariMilele FmSwahili

Wanafunzi waliojiunga na shule za upili za kitaifa wanaosoma na kurejea nyumbani waanza kujiunga na kidato cha kwanza leo

Wanafunzi waliopata nafasi katika shule za upili za kitaifa kama wanaosoma na kurejea nyumbani wanaanza kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule hizo leo. Wizara ya elimu imeziagiza shule za kitaifa kuwapokea wanafunzi hao kuanzia leo hadi jumatatu wiki ijayo. Shule zinazowapokea wanafunzi hao ni Kenya High Starehe Moi Forces Academy na Lenana. Zingine ni shule ya upili ya wasichana ya Pangani ile ya Moi hapa Nairobi shule za upili za wasichana ya Ngara Buruburu, Embakasi Nembu St Georges na Statehouse. Wanafunzi hao pia watajiunga na shule za Arya Parklands, Dagoretti Lang’ata Upper Hill, Hospital Hill na Ofafa Jericho. Serikali ilianzisha mpango wa wanafunzi kusoma katika shule hizo ili kukabili changamoto za uhaba wa nafasi za mabweni wakati ongezeko la wanafunzi likitarajiwa kutokana na utekelezaji mpango wa elimu bila malipo katika shule za upili.

Show More

Related Articles