Pilipili FmPilipili FM NewsSwahili

Meli Ya MS Nautica Yaongeza Matumaini Ya Utalii Kuimarika Nchini.

Meli hii ya kifahari ya MV Nautica kutoka  nchi ya Norway Imewasili katika bandari ya Mombasa mapema leo ikiwa na jumla watalii 900.

Meli hii inakua ya nne kutia nang’a bandarini humo kwa kipindi cha miezi minne ilyopita na ikiwa meli ya kwanza kuwasili nchini chini ya siku nne mwaka huu wa 2018.

Kama anavyoelezea mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika halimashauri ya bandari Haji Masemo , kuimarika kwa usalama nchini kabla ,wakati na baada ya uchaguzi ndio kiini cha kuimarika kwa utalii humu nchini.

Show More

Related Articles