HabariMilele FmSwahili

Muungano wa NASA watarajiwa kutangaza mikakati ya kubuni mabunge ya halaiki na hatua walizoafikia

Muungano wa NASA unatarajwia kutangaza mikakati yake kuhusu kubuniwa mabunge ya halaiki na hatua ambazo wameafikia. Hii ni baada ya muungano huo kuhairisha mipango ya kuapishwa kwa Raila Odinga na Kalonzo Musyoka. Mkutano wa leo utatumiwa na kamati iliyobuniwa kuongoza harakati za kubuni mabunge hayo inayoongozwa na mwanastrategia David Ndii, kuweka bayana mwelekeo ambao NASA itachukua. Mkutano huo aidha unakujia siku chache tu baada ya Kalonzo kusema huenda ataapishwa pamoja na Raila iwapo hakutakwua na mazungumzo yoyote baina yao na rais Uhuru Kenyatta. Hata hivyo vitisho hivi vimekuwa vikitupiliwa mbali na wanasiasa wa Jubile wanaodai hakuna la mno kutoka kwa wana NASA.

Show More

Related Articles