HabariPilipili FmPilipili FM News

Afueni Kwa Nyong’o. Baada Ya Mahakama Kufutilia Kesi Dhidi Yake

Mahakama kuu imetupilia mbali kesi ya aliyekuwa gavana wa kisumu Jack Ranguma ambaye alikuwa anapinga ushindi wa gavana wa sasa Professa Anyang Nyong’o.

Aidha mahakama hiyo imemtaka ranguma  kulipa gharama ya kesi hiyo ya kima cha shilingi milioni 5.

Katika uamuzi wake jaji David Majanja ametupilia mbali hoja nyingi za Ranguma ikiwemo madai ya wizi wa kura pamoja na kukosa kujumuishwa kwa matokeo ya vituo vitano akisema matukio ya vituo hivyo hayangeweza kuathiri matokeo ya mwisho ya ugavana.

 

Waliokuwa kinyume cha kesi hiyo ni tume ya uchaguzi nchini IEBC, gavana wa kisumu Anyang Nyongo pamoja na afisa rejeshi wa kaunti hiyo.

Ranguma aliwasilisha kesi hiyo akipinga ushindi wa gavana nyong’o kwenye uchaguzi wa agosti 8 kwa msingi kuwa uchaguzi huo uliingia dosar

Show More

Related Articles