HabariPilipili FmPilipili FM News

Wizara Ya Elimu Iko Tayari Kutekeleza Mfumo Mpya Wa Elimu

Waziri wa Elimu Daktari Fred Matiangi ameongoza kikao cha wadau wa elimu leo ili kutathmini  namna ya kuutekeleza mtaala mpya wa elimu

Akizungumza baada ya kikao hicho matiangi amedokeza kuwa wizara ya elimu iko tayari kutekeleza mtaala huo mpya huku akiongeza kuwa mfumo huo utahusisha shule za uma nazile za kibinafsi kuanzia ngazi za chini, akisema tayari wameanzisha mafunzo maalum kwa walimu.

Matiangia aidha amefutilia madai kuwa hakutakua na mtihani wa kitaifa wa KCPE akieleza kuwa mtawala  huu mpya utaanza kutekelezwa kikamilifu mwaka wa 2027 katika ngazi zote za elimu.

Kwa Upande wake mwenyekiti wa taasisi ya mitaala ya elimu nchini KICD Daktari Sarah Ruto amesema mikakati yote kuhusiana na mfumo huu mpya imekamilika.

Mkutano huo unafanyika  siku moja tu baada ya shule kufunguliwa kwa muhula wa kwanza wakati kukiwa na mkanganyiko kuhusu utekelezaji wa mtaala huo mpya

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker