HabariPilipili FmPilipili FM News

Magari Ya Pigwa Mnada Katika Bandari Ya Mombasa

Madalali  na wafanyibiashara leo wameshiriki mnada wa bidhaa ambazo wamiliki wake walishindwa kulipa ushuru waliotakiwa kulipia bidhaa hizo katika Bandari ya Mombasa.

Shughuli hiyo inafuatia ilani iliyowekwa katika gazeti rasmi la serikali, ikiwaonya walioagiza mali hizo kwamba iwapo wangekosa kujijtokeza kwa kipindi cha siku 30 mali zao zitapigwa mnada.

Baadhi ya mali ambazo zimepigwa  mnada  ni pamoja na magari, vifaa vya kujengea, vifaa vya nyumbani zikiwemo jokofu na runinga miongoni mwa vingine.

Zoezi hilo limesimamiwa na mamlaka ya ukusanyaji na utozaji ushuru nchini KRA huku zoezi lingine kama hilo likitarajiwa kufanyika tarehe 17 ya mwezi huu wa januari

Show More

Related Articles