HabariMilele FmSwahili

Kinamama wajawazito hawatahudumiwa katika hospitali ya Kenyatta bila bima ya NHIF

Kinamama wajawazito ambao hawajajisajili kama wanachama wa bima ya afya NHIF hawatahudumiwa katika hosipitali ya Kenyatta. Kaimu afisa mkuu Dr.Benerd Gitahe ameagiza kila mama mjamzito kujisajili kwa NHIF kabala ya kuhudumiwa hosipitalini humo. Kwenye barua kwa wafanyikazi wote, Githae ameeleza uamuzi huo ni kufuatia hatua ya serikali kubadili mpango wa kujifungua bila malipo kuwa chini ya hazina ya ‘linda mama’ iliyozinduliwa na rais Uhuru Kenyatta mwezi Oktoba mwaka 2016. Sasa itabidi kinamama wajawazito kulipa shilingi 500 kila mwezi huku Githae akiongeza kuwa agizo hilo litarahisisha taratibu za hosipitali hiyo kupata malipo kutoka kwa NHIF kwa muda unaofaa.

Show More

Related Articles