HabariMilele FmSwahili

Watu kadhaa wajeruhiwa kwenye ajali eneo la Kayole mjini Naivasha

Watu kadhaa wamejeruhiwa vibaya baada ya basi kugongana na matatu katika eneo la Kayole mjini Naivasha katika barabara ya Nairobi Nakuru. Basi hilo la abiria lilikuwa likitoka hapa Nairobi kuelekea Busia. Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Naivasha. Yakijiri hayo baraza la mashirika yasiyokuwa ya serikali limeunga mkono marufuku kwa magari ya uchukuzi kuhudumu nyakati za usiku. Mwenyekiti Stephen Cheboi hata hivyo ameitaka serikali kupitia idara husika kuweka mkakati kabambe wa kudhibiti ajali za barabarani.
Show More

Related Articles