HabariMilele FmSwahili

Nyongo apata afueni baada ya mahakama ya Kisumu kutupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wake wa Agosti 8

Gavana wa Kisumu Anyang Nyongo amepata afueni baada ya mahakama kuu mjini humo kutupilia mbali kesi ya kupinga kuchaguliwa kwake mnamo Agosti nane mwaka jana. Jaji David Majanja katika uamuzi wake amesema hakuna ushahidi kudhibitisha madai ya wizi wa kura. Pia jaji Majanja ametupa madai ya kutojumuishwa matokeo ya kura kutoka vituo vitano akisema kura hizo haziwezi kubadilisha matokeo ya uchaguzi. Mahakama pia imemwagiza mlalamishi aliyekuwa gavana Jack Ranguma kulipa shilingi milioni 2.5 kama gharama ya kesi.

Show More

Related Articles