HabariMilele FmSwahili

Asilimia 64 ya wakenya waeleza imani kuwa mwaka huu utakua mwema kuliko 2017

Asilimia 64 ya wakenya wameelezea imani kuwa mwaka huu utakuwa mwema kuliko 2017. Kwa mujibu wa utafiti wa shirika la taifa asilimia 17 ya wananchi hawana uhakika kuhusu hali itakavyokuwa huku asilimia 14 wakihisi mwaka huu utakuwa mgumu kuliko mwaka jana. Aidha zaidi ya asilimia 75 ya wafuasi wa Jubilee wanaimani mwaka huu utakuwa bora huku asilimia 50 ya wafuasi wa NASA wakisema wanatarajia mema. Utafiti huo pia umebaini kuwa asilimia 32 ya wakenya wanaazimia kuanzisha biashara mwaka huu, asilimia 24 wakitarajia kupata ajira nao asilimia 24 wakilenga kuendelea na masomo.

Show More

Related Articles