HabariMilele FmSwahili

Watu wanne wauawa kufuatia shambulizi la Alshabaab kwa gari la polisi huko Mandera

Watu wanne wameuawa baada ya washukiwa wa kundi la kigaidi la Al shabbab kushambulia gari la polisi wa utawala katika eneo la Gamurey kati ya Kutulo na Qorofqarar kaunti ya Mandera. Waliouwawa ni polisi mmoja wa utawala wawili wa ziada na mtu mmoja. Watu wanne wamelazwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Kutulo. Watu wengine tisa wameripotiwa kutoweka. Aidha washambuliaji wameteketeza gari hilo la polisi.

Show More

Related Articles