HabariPilipili FmPilipili FM News

Kamati Ya Usafiri Bungeni Yapendekeza Magari Ya Mizigo Yatafutiwe Njia Mbadala

Mwenyekiti wa kamati ya usafiri bungeni David Pkosing amependekeza magari ya mizigo kutafutiwa njia mbadala badala ya kutumia barabara za Nakuru-Eldoret na ile ya kisumu, hiyo ikiwa njia moja ya kupunguza ajali nyingi zinazoshuhudiwa humu nchini.

Mbunge huyo wa pokot Kusini anasema ajali zinashuhudiwa kwa wingi katika maeneo yaliyo na magari mengi ya mizigo hususan Trela.

Pkosing amependekeza magari ya mizigo yanayoelekea kisumu yatumie barabara ya Molo huku yale yanayoelekea Eldoret yatumie barabara ya Eldama Ravine wakati kukisubiriwa ujenzi wa barabara ya pande mbili.

Watu 36 walifariki siku ya jumapili na wengine 18 kujeruhiwa pale basi moja la abiria liligongana ana kwa ana na Trela eneo la migaa katika barabara ya Nakuru – Eldoret.

Show More

Related Articles