HabariPilipili FmPilipili FM News

Wananchi Wa Waombwa Kutowatenga Wafungwa Wanaorudi Katika Jamii

Jamii katika kaunti ya Taita Taveta imetakiwa kutowatenga waliokuwa wafungwa na ambao wamerekebisha tabia na kurejea mitaani na badala yake kuwaonyesha upendo.

Ni usemi wa Charles Ogur afisa anayesimamia gereza la Wundanyi ambaye anasema kuwatenga wafungwa wanaorudi katika jamii huwafanya kujiona wapweke, hali ambayo huchangia baadhi yao kurejelea uhalifu na kurudishwa gerezani.

Ogur ameyasema haya wakati wa kuwatembelea wafungwa katika gereza la wundanyi ili nao wajihisi kukumbukwa.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker