HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Sportpesa yaondoa ufadhili

Kampuni ya kamari ya kubashiri matokeo ya mechi Sportpesa, imesitisha udhamini wake kwa michezo nchini wa thamani ya shilingi milioni 600 kuanzia leo.
Hii ni baada ya mahakama kuu kutupilia mbali ombi la Sportpesa dhidi ya kubatilisha kodi ya asilimia 35 inayotozwa mapato ya ujumla ya kampuni za bahati nasibu na kamari kwa misingi kuwa ushahidi uliotolewa haukuwa wa kutosha.
Kwa mujibu wa Sportpesa, hatua hii ni mojawapo ya mipango inayofanywa na kampuni yenyewe ili kupunguza gharama ya matumizi huku ikisubiri kukata rufaa.

Show More

Related Articles