MichezoPilipili FmPilipili FM News

SportPesa Yajiondoa Kama Wadhamini Wa Michezo Nchini.

Kampuni ya mchezo wa bahati nasibu ya Sport Pesa imetoa rasmi udhamini wake kwa timu za humu nchini baada ya wiki iliyopita kupoteza kesi waliowasilisha mahakamani wakilalamikia ushuru mkubwa wa asilimia 35 wanaotozwa na serikali.

Akizungumza leo mkurugenzi mkuu wa Sport Pesa nchini Ronald Karauri amesema itakua vigumu kwa wao kutekeleza kazi zao pamoja na kudhamini timu nchini kutokana na kutozwa kiwango kikubwa cha ushuru.

Awali kampuni hio ilitishia kujitoa kama wadhamini kabla ya kuelekea mahakamani.

Timu ambazo zitaathirika kutokana na kujiondoa kwa sport pesa ni pamoja na Gor Mahia, AFC Leopards timu ya raga wachezaji saba kila upande, mashirikisho ya ndondi pamoja na lile la soka la FKF bila kusahau usimamizi wa timu ya taifa harambee stars.

Lakini hata hivyo serikali kupitia wizara ya michezo imeahidi kuwaalika washikadau wote katika meza ya mazungumzo kujadiliana kuhusiana na swala hilo

Akiongea mjini Mombasa katibu katika wizara ya michezo Kirimi Kaberia amesema ana imani mwafaka utapatikana.

Show More

Related Articles