HabariMilele FmSwahili

Cleophas Malala: Raila atazindua bunge la halaiki kaunti ya Kakamega tarehe 7 mwezi huu

Seneta wa kaunti ya Kakamega Cleophas Malala anasema kinara wa NASA Raila Odinga atazindua bunge la halaiki katika kaunti ya Kakamega tarehe 7 mwezi huu. Akiongea huko Sherere kaunti ya Kakamega Malala anasema ni kupitia mabunge hayo ambapo kinara wa NASA Raila Odinga na naibu wake Kalonzo Musyoka wataweza kuapishwa. Ameendelea kulaumu serikali ya Jubilee akisema imekuwa ikitoa ahadi ambazo si za kweli kwa wananchi wakati wa kampeni.

Show More

Related Articles