HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Bamburi Waombwa Kushirikiana Na Viongozi Wao

Mwakilishi wa wadi ya Bamburi Robert Nyiro amewataka wakaazi wa eneo hilo kuwa na ushirikiano wa karibu na viongozi wao ili waweze kupata maendeleo ya haraka iwezekanavyo.

Akiongea na waandishi wa habari katika fainali ya michuano ya kuwania taji la Nyiro Cup katika uwanja wa Utange, kiongozi huyo amesema eneo hilo linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa Ukumbi wa jamii.

Ameitaja hali hiyo kuwanyima fursa vijana na makundi ya kinamama, kufanya mikutano yao na kuboresha talanta zao  mashinani.

Show More

Related Articles