HabariPilipili FmPilipili FM News

Magavana Waahidi Kupatia Kipao Mbele Miradi Ya Maendeleo

Magavana wameahidi kupatia kipao mbele miradi ya maendeleo mwaka huu katika juhudi zao za kuwahudumia wananchi.

Kufikia sasa magavana wengi bado hawajaweza kutekeleza ahadi walizoahidi kuzitekeleza chini ya siku 100, ikiwemo kuweka msingi wa huduma za msingi pamoja na kujaza nafasi wazi za maafisa wa kaunti kupitia uteuzi.

Kando na hayo imebainika kuwa mgao wa kaunti kutoka kwa serikali kuu bado hautoshi jambo ambalo magavana wanasema wanashauriana jinsi ya kulitatua

Show More

Related Articles