HabariMilele FmSwahili

Muungano wa wahudumu wa matatu wataka NTSA kufanyiwa mabadiliko

Muungano wa wahudumu wa matatu nchini umetaka kufanyiwa mabadiliko na kupigwa msasa kwa maafisa wasimamizi wa mamlaka ya usalama barabarani NTSA. Mwenyekiti wake Dickson Mbugua anasema NTSA imefeli katika kutekeleza majukumu yake kufuatia kukithiri kwa visa vya ufisadi miongoni mwa wasimamizi wake anaosema wanashirikiana na polisi wa trafiki kuchukua hongo. Kupitia mweka hazina wake Lucy Mathenge muungano huo umekosoa agizo la NTSA kupiga marufuku usafiri wa usiku wakisema hatua hiyo haifai.

Show More

Related Articles