People Daily

Msongamano Wa Abiria Wazidi Kushuhudiwa

Msongamano wa abiria unaendelea kushuhudiuwa kwa siku ya tatu mfululizo katika vituo vingi vya mabasi hasa katika miji ya mombasa, Nairobi na kisumu, kufuatia marufuku ya serikali inayozuia magari hayo kusafiri nyakati za usiku.

Baadhi ya abiria hapa mombasa, wameilamu mamlaka ya  NTSA kwa kuweka marufuku hiyo bila ilani yoyote wakisema imeathiri safari zao pakubwa.

Wamiliki wa magari hayo wameiomba serikali kutathmini marufuku iliyowekwa dhidi yao, wakisema huenda ikalemaza shughuli muhimu kwa wananchi hasa wakati huu ambapo watoto wanarudi shuleni

Show More

Related Articles