HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Mfumo mpya wa elimu, 2-6-6-3 kuzinduliwa

Huku masomo yakitarajiwa kurejelewa shuleni hapo kesho kufuatia likizo ndefu wanafunzi kote nchini haswa wale wa shule za chekechea wanatarajiwa kuwa waanzilishi wa mtaala mpya wa elimu wa 2-6-6-3, ambao unatarajiwa kuimarisha elimu nchini.

Mtaala huo mpya utashuhudia wanafunzi wakisoma kwa miaka miwili katika shule ya chekechea, miaka sita shule ya msingi, miaka mitatu, awamu ya chini ya shule ya upili, na miaka mingine mitatu katika awamu ya juu ya shule ya upili, na kisha kutamatisha mafunzo katika chuo kikuu kwa miaka mitatu.

Ikitofautishwa na mtaala wa -8-4-4, mtaala huu mpya unatarajiwa kulenga msingi wa utendakazi na vipaji kwa wanafunzi.

Mtaala huu mpya pia utaanzisha mtihani wa kutathmini utendakazi na vipawa vya wanafunzi.

Show More

Related Articles