HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwaka Ulio Pita Watajwa Kuwa Mgumu Zaidi

Huku sherehe za mwaka mpya zikiendelea katika maeneo mbali mbali ya dunia, humu nchini idadi kubwa ya wakenya walikesha katika sehemu za burudani na makanisa, katika shamrashamra za kuukaribisha mwaka mpya.

Wengi tulioweza kuzungumza nao hapa mombasa wameutaja mwaka wa 2017 kuwa mgumu zaidi kutokana na changamoto nyingi walizoshuhudia.

Baadhi wameeleza siasa na uchaguzi pamoja na kupanda kwa gharama ya maisha kama baadhi ya mambo yaliochangia changamoto kwa wakenya, huku wakionyesha matumaini ya hali kubadilika mwaka huu mpya wa 2018.

 

Show More

Related Articles