HabariPilipili FmPilipili FM News

Madereva Waombwa Kuwa Wangalifu Barabarani

Maderva wameombwa kuwa wangalifu barabarani ili kupunguza idadi ya ajali zinazo sababisha maafa kwa wakenya.

Mwito huu umetolewa na Askofu mstaafu wa kanisa la kianglikana jimbo la Mombasa JULIUS  KALU, ambaye ameunga mkono hatua ya mamlaka ya Usafiri na usalama barabarani NTSA  kupiga marufuku safari za magari ya uma ya mwendo mrefu masaa ya usiku.

Kiongozi huyo wa kindini amewataka wananchi na viongozi kushirikiana pamoja na kutohusisha mwaka huu wa 2018 na siasa mbaya kama zilizoshuhudiwa mwaka jana ili taifa liweze kupiga hatua kimaendeleo.

Kalu alikuwa akizungumza katika kanisa la Ack Cathedral hapa jijini Mombasa alipo kuwa akifinya ibada yake ya Mwisho Kama Askofu wa kanisa hilo, baada ya kulitumikia kwa muda wamiaka 37 .

Show More

Related Articles