HabariMilele FmSwahili

Watu 12 wauwawa kwenye ajali ya ndege magharibi mwa Costa Rica

Watu 12 wameuwawa kwenye ajali ya ndege magharibi mwa Costa Rica. Kumi kati ya wale waliouwa walikuwa ni raia wa Marekani akiwemo rubani raia wa Costa Rica na rubani msaidizi. Vyombo vya habari vilisema kuwa watano kati ya wale waliouawa walitoka familia moja. Ndege hiyo aina ya Cessna 208 ilikuwa safarini kutoka mji mkuu San José. Hakukuwa na manusura na wala haibainiki ni nini kilisababisha ajali hiyo.

Show More

Related Articles