HabariMilele FmSwahili

KDF wauwa waasi 5 wa kundi la Alshabaab

Wanajeshi wa KDF wamewauwa waasi 5 wa kundi la Alshabaab wakati wa oparesheni ya kuwasaka waasi waliovamia kambi ya polisi ya ijara kaunti ya Garissa. Polisi walipata silaha kadha kutoka kwa wahusika ikiwemo bunduki 5 aina ya Ak47 na zaidi ya risasi 130. Msemaji wa KDF David Obonyo anasema baadhi ya washukiwa wametoweka na majeraha ya risasi kuelekea eneo la Sarira .Anasema wanajeshi hao walinasa washukiwa walipokuwa wakielekea katika mpaka wa Somalia.

Show More

Related Articles