HabariPilipili FmPilipili FM News

Abiria Walazimika Kukesha Katika Vituo Vya Mabasi

Mamia ya abiria wamelazimika kukesha katika vituo vya mabasi ya mwendo mrefu katika miji ya mombasa, Nairobi na kisumu, kufuatia marufuku ya serikali inayozuia magari hayo kusafiri nyakati za usiku.

Baadhi ya abiria hapa mombasa wameilamu mamlaka ya NTSA kwa kuweka marufuku hiyo bila ilani yoyote kwa kile wanadai imeathiri safari zao pakubwa.

Wamiliki wa magari hayo wameiomba serikali kutathmini marufuku iliyowekwa dhidi yao wakisema huenda ikalemaza shughuli muhimu kwa wananchi hasa wakati huu ambapo watoto wanarudi shuleni.

Baadhi wametaka marufuku hiyo iwekwe kwa magari ya mizigo ikiwemo matrela kwa madai kuwa magari hayo ndio husababisha ajali nyakati za usiku.

Kulingana na marufuku iliyotolewa hapo jana na mamlaka ya usalama na usafiri wa  barabarani NTSA ,mabasi ya mwendo mrefu yataruhusiwa tu kusafiri kati ya saa kumi na mbili asubuhi na saa moja jioni ikiwa ni katika juhudi za kupunguza ajali zinazoshuhudiwa humu nchini.

Show More

Related Articles