HabariMilele FmSwahili

Tahadhari yatolewa kufuatia ongezeko la saratani eneo la South Rift

Tahadhari imetolewa kufuatia ongezeko la visa vya saratani eneo la South Rift, hususan kwenye kaunti za Kericho na Bomet. Wenyeji, wakiongozwa na Jackson Rotich wanasema visa hivyo vimeongezeka ikilinganishwa na hapo awali, hali ambayo imewatia hofu. Wenyeji hao aidha wamelalamikia gharama ya juu ya matibabu huku wakitoa mwito kwa serikali kuu na zile za kaunti kushirikiana ili kufanikisha vita dhidi ya ugonjwa huo. Afisa wa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Kericho Ruth Cheruiyot, hata hivyo amewashauri wenyeji kupimwa saratani kila mara ili kurahisisha matibabu endapo watapatikana na ugonjwa huo.

Show More

Related Articles