HabariK24 TvSwahiliVideos

Masaibu wanayopitia makahaba katika kujikinga na Ukimwi

Ijapokuwa vita dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi vimeimarishwa nchini, juhudi hizo zinazidi kulemazwa na idadi ya maambukizi baina ya kundi la watu linalojumuisha makahaba, mabasha na waraibu wa dawa za kulevya miongoni mwa wengine  huku utafiti ukionyesha kuwa walio kwenye hatari hata zaidi ni makahaba.

hata hivyo, japo kuwa kaunti ya meru ambayo ni mojawapo ya kaunti  ambazo idadi ya  maambukizi ya virusi vya ukimwi iko juu miongoni mwa wanawake kuliko wanaume  kwa asilimia 3.9% na 1.7 % mtawalia, kaunti hiyo sasa imeimarisha mikakati yake ya kukabiliana na janga hilo mingoni mwa makahaba kwa kuwahamasisha kuhusu ugonjwa wa Ukimwi na kuwapa mipira ya ngono jambo amabalo sasa kaunti hiyo inasema limesaidia kupunguza idadi ya maambukizi baina ya makahaba katika kaunti hiyo.

Show More

Related Articles