HabariMilele FmSwahili

Watalii Wengi humu nchini wakosa fursa ya kusherehekea siku ya kufunga mwaka nje ya miji yao

Huenda watalii wengi wa humu nchini wakakosa kusherehekea siku ya kufunga mwaka ambayo ni tarehe 31 ya mwezi huu nje ya miji yao. Hali hii imehusishwa na kufunguliwa kwa shule za umma tarehe 2 ya mwezi wa Januari mwakani. Meneja wa mauzo katika hoteli ya Travellers Bonface Wafula anasema hali hii imechangia wageni wengi waliokuja kaunti ya Mombasa kujivinjari kuondoka mapema. Wafula ametoa wito kwa waziri wa elimu Daktari Fred Matiangi kuangazia kufanya mabadiliko kwenye kalenda ya shule zote za umma.

Show More

Related Articles