HabariMilele FmSwahili

Muungano wa wafanyibiashara wawasilisha kesi mahakamani kupinga marufuku dhidi ya shisha

Muungano wa wafanyibiashara wa shisha umeelekea mahakamani kupinga marufuku dhidi ya uagizaji na uuzaji wa shisha. Katika kesi iliowasilishwa mahakama ya Milimani hapa Nairobi, wafanyibiashara hao wanadai marufuku hiyo haiambatani na sheria na kwamba iwapo itatekelezwa huenda ikaathiri biashara yao. Pia wanadai marufuku hiyo itapelekea vijana wengi kupoteza ajira na wanalenga kuiomba mahakama kubatili marufuku hiyo iliotangazwa jana na waziri wa afya Cleopa Mailu. Tayari marufuku hiyo ilikua imeanza kupokea uungwaji mkono, viongozi wa dini wakiongozwa na Abubakar Bini  na Elijah Kiambati wakiitaka serikali kutolegeza kamba katika utekelezwaji wa marufuku hiyo.

Show More

Related Articles