HabariPilipili FmPilipili FM News

George Weah Kutangazwa Kama Rais Mteule Wa Liberia

George Weah Leo atatangazwa kuwa rais mteule wa Liberia na tume ya uchaguzi nchini humo, baada ya kuongoza kwa asilimia 61.5 ya kura zote zilizohesabiwa.

Weah amemtangulia mpinzani wake mkuu Joseph Boakai  kwa asilimia 60 ya kura zilizopigwa.

Anachukua nafasi ya mwanamke wa kwanza barani Afrika kuwa rais Bi.Ellen Johnson Sirleaf, anayemaliza muda wake kwa mjibu wa katiba ya nchi hiyo na ambaye pia ni mshindi Tuzo ya Nobel.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza taifa hilo kupata kiongozi kwa njia ya kidemokrasia.

Rais Uhuru Kenyatta ni kati ya viongozi ambao wametuma jumbe za pongezi kwa George Weah kwa kushinda uchaguzi wa kiti cha urais Nchini Liberia.

Kupitia ujumbe, katika ukurasa wa mtandao wake wa Twitter rais Kenyatta pia amewapongeza wananchi wa Liberia kwa kufanikisha uchaguzi wa  huru na amani

Show More

Related Articles