HabariMilele FmSwahili

Hifadhi ya Maiti ya Kakamega yawataka wenyeji kuichukua miili ya wapendwa wao iliyorundika humo

Usimamizi wa hifadhi ya maiti ya Kakamega unawataka wenyeji kuichukua miili ya wapendwa wao iliorundikana katika chumba hicho. Afisa wa afya ya umma katika hospitali ya rufaa ya Kakamega Mustafa Yusuf anasema baadhi ya miili hizo ziliokotwa barabarani na polisi kwa muda wa miezi mitano iliyopita. Anasema kurundika kwa miili hizo ni tishio kwa afya ya maafisa wanaohudumu katika chumba hicho na pia zinasababisha msongamano kupelekea kuwepo kwa uhaba wa nafasi. Ameongeza kuwa tayari wamepata kibali cha kuzika miili 18 huku wakipania kutafuta kibali cha kuzika miili zaidi iwapo wenyeji hawatojitokeza.

Show More

Related Articles