HabariPilipili FmPilipili FM News

Mifugo wa Tatiza shughuli za usafiri Malindi

Wahudumu Wa piki piki mjini Malindi kaunti ya Kilifi wamelalamikia kuongezeka kwa mifugo katikati mwa mji hasa kwenye barabara za mji huo.

Wakiongozwa na Said Mohamed wamedokeza kuwa suala hilo limekuwa kero kubwa ikizingatiwa kuwa linachangia msongamano wa magari hasa msimu huu wa sherehe.

Sasa wahudumu hao wanahofia kuwa huenda hali hiyo ikachangia ajali za barabarani na hivyo kuiomba serikali ya kaunti kuingilia kati na kuwachukulia hatua wamiliki wa mifugo hiyo.

Hata hivyo tayari idara  ya ustawi Wa mifugo kata ndogo ya Malindi imewaonya jamii wanaofuga ng’ombe kuwa waangalifu, ili mifugo yao isitatize Mbarabarani.

Show More

Related Articles