HabariMilele FmSwahili

Shughuli za kawaida zatatizika katika hosipitali ya St Mary’s hapa Nairobi

Shughuli za kawaida zimetatizika katika hosipitali ya St.Mary’s hapa Nairobi baada ya polisi kuwatimua wagonjwa na wafanyikazi waliokua ndani. Hatua hiyo inadaiwa kutekelezwa kufuatia mzozo unaozingira umiliki wa hosipitali hiyo baina ya watawa wa Marie Theresa Gathambi na Padiri raia wa Uingereza William Charles. Inadaiwa watawa hao waliagiza polisi kuzingira hosipitali hiyo na kuwaondoa waliokua ndani pasi na kuruhusu yeyote kuingia. Wagonjwa waliokua wanapokea matibabu wameelezea jinsi walivyofurushwa na polisi waliojihami kuanzia mwendo wa saa kumi asubuhi huku waliotaka kuingia ndani wakizuiwa. Umiliki wa hosipitali hiyo pamoja na ile ya Nakuru umekumbwa na utata kwa miaka mitano iliopita. Padiri William alielekea mahakamani kutaka kiongozi wa kanisa katoliki kadinali John Njue kuzuiwa kumlazimu kuruhusu hosipitali hizo kumilikiwa na watawa hao.

Show More

Related Articles