HabariMilele FmSwahili

Mfumo mpya wa elimu kutekelezwa kwa wanafunzi wa darasa la 1 na 2 kuanzia mwaka ujao

Mfumo mpya wa elimu utaanza kutekelezwa kwa wanafunzi watakaojiunga na darasa la kwanza na lile la pili mwaka ujao, ambazo sasa zitakuwa masomo ya chekechea ukipenda Pre Primary 1 na Pre Primary 2. Baadaye watafanya mtihani wa kujiunga na Grade 1, kabla ya kuendelea na masomo hadi Grade 3 ambapo watakamilisha elimu ya lower primary. Upper primary itaanzia Grade 5 hadi Grade 6 ambayo ni sawa na darasa la nane chini ya mfumo wa 8-4-4. Masomo ya shule ya upili yataanzia Grade 7 hadi Grade 9 lakini kwa kiwango cha chini (Junior High School). Mwanafunzi akikamilisha atakuwa huru kuchagua iwapo atajiunga na chuo cha kiufundi ama ataendelea na kiwango cha juu cha masomo ya sekondari (Senior High School) ambayo ni Grade 10, 11 na 12. Wanaokamilisha kiwango hicho wanajiunga na vyuo vikuu. Wanafunzi wote wanaoingia darasa la tatu hadi darasa la nane hawataathiriwa na mfumo huu mpya.

Show More

Related Articles