HabariPilipili FmPilipili FM News

Maombi Ya Kila Mwaka Ya Kuombea Taifa Ya Endelea Huko Mlima Kenya

Waumini kutoka tabaka mbalimbali kote nchini wanafanya maombi yao maalum ya kila mwaka ambayo hujumuisha zoezi la kuuzunguka mlima kenya mwishoni mwa mwezi wa disemba kila mwaka.

Kulingana na waandalizi wa hafla hiyo, maombi ya mwaka huu ni kumshukuru Mungu kwa ajili ya taifa la kenya kwa kudumisha amani na utulivu katika msimu wote wa kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi.

Maombi haya yanafanyika wakati wito ukiendelea kutolewa kwa viongozi wakuu serikalini na upinzani kuandaa mazungumzo ya taifa kwa ajili ya kumaliza mgawanyiko wa kisiasa uliotokana na uchaguzi

Show More

Related Articles