HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakimbizi Zaidi Kutoka Congo Wakimbilia Uganda

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa zaidi ya wakimbizi 4,500 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekimbilia nchini Uganda.

Filippo Grandi Mkuu wa Shirika hilo ametangaza kuwa wengi wa wakimbizi hao wameingia Uganda kupitia ziwa Albat.

Taarifa zaidi kutoka shirika hilo inasema wakimbizi zaidi ya 1,860 wamesajiliwa kati ya tarehe 23 hadi 26 mwezi huu wa Disemba na hivyo kuifanya idadi ya wakimbizi waliowasili nchini Uganda tangu tarehe 18 mwezi huu kufikia 4,584.

Show More

Related Articles