Pilipili FmPilipili FM NewsSwahili

Watu 7 Wafariki Kwenye Ajali Sultan Hamood.

Inaarifiwa ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa nne baada ya magari hayo mawili kugongana ana kwa ana katika eneo la Kilimbini barabara kuu ya Mombasa Nairobi leo asubuhi.

Kamishna wa kaunti ya makueni Maalim Mohamed amethibitisha tukio hilo akisema huenda idadi ya vifo ikaongezeka, ikizingatiwa kuwa baadhi ya watu walipata majeraha mabaya.

Kufikia sasa zaidi ya watu 200 wamepoteza maisha kwenye ajali za barabarani mwezi huu wa disemba pekee, huku kidole cha lawama kikielekezwa kwa maafisa wa trafiki na madereva kwa kutokuwa makini.

 

Show More

Related Articles