HabariK24 TvSwahiliVideos

Hakimu wa Kwale Doreen Mulekyo alijiokoa baada ya kutekwa nyara

Muungano wa majaji na mahakimu nchini unamtaka inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinett kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusiana na kutekwa nyara kwa hakimu mmoja katika eneo la diani kaunti ya Kwale.
Muungano huo umesema ulinzi wa kutosha unafaa kupewa majaji na mahakimu, hususan kutokana na hatari ambayo mara nyingi huwakodolea macho.
Hakimu mkuu wa mahakama ya kwale Doreen Mulekyo alitekwa nyara na watu wasiojulikana lakini akafanikiwa kujiokoa baada ya kuruka kutoka kwa gari alimokuwa kama anavyotuarifu Kiama Kariuki.

Show More

Related Articles