HabariPilipili FmPilipili FM News

Msongamano Wa Wasafiri Wa Shuhudiwa Mjini Mombasa

Huku sherehe za krismasi na mwaka mpya zikikaribia shughuli za uchukuzi hapa mjini Mombasa  zimeshika kasi.

Msongamano msongamano mkubwa wa wasafiri unashuhudiwa katika vituo mbali mbali vya mabasi hapa mjini Mombasa jambo ambalo limesababisha nauli ya mabasi kupandishwa zaidi.

Hata hivyo wasafiri wanaoelekea jijini Nairobi wametajwa kupungua  kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miaka ya hapo awali.

Kwa sasa wasafiri wameshauriwa kukata tikiti zao mapema ili kuepuka matatizo siku ya kusafiri.

Show More

Related Articles