HabariMilele FmSwahili

Matokeo ya KCSE mwaka huu yaibua hisia mseto

Wadau katika sekta ya elimu wanaendelea kutoa hisia mseto kuhusiana na shinikizo la kufutiliwa mbali matokeo ya mtihani wa KCSE mwaka huu. Waziri wa elimu katika kaunti ya Nairobi Janet Muthoni Ouko amepinga pendekezo la kufutuliwa mbali matokeo hayo akisema halifai. Amesisitiza haja ya kuzingatiwa juhudi zilizowekwa na serikali kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata alama wanazostahili katika mtihani. Pia ameonya dhidi ya kuingizwa siasa katika jitihada za kuboresha sekta ya elimu nchini.

Show More

Related Articles