HabariK24 TvSwahiliVideos

Mwanafunzi ajitoa uhai Migori kwa kupata alama ya ‘C-‘ kwenye KCSE

Mwanafunzi mmoja wa kike amejitia kitanzi baada ya kupata alama ya C –  katika mtihani wa kidato cha nne KCSE mwaka huu ambao matokeo yalitangazwa hapo jana na waziri wa elimu Fred Matiang’i.

Kulinganna na familia yake  Caren Onyango mwenye umri wa miaka 22 alipoteza matumaini baada ya kupata alama sawa na aliyokuwa amepata miaka miwili iliyopita aliporudia darasa hilo katika shule ya upili ya wasichana ya Moi Nyabohanse eneo bunge  la Kuria magharibi kaunti ya  Migori.

Show More

Related Articles