HabariMilele FmSwahili

Wabunge wapitisha mswada wa kuondoa kikomo cha umri wa rais Uganda

Wabunge walipitisha kwa wingi sheria ya kuruhusu kuwe na rais mwenye umri wowote na hivyo kutoa nafasi kwa Rais Yoweri Museveni kuwania wadhifa huo ahudumu kipindi cha sita madarakani. Mswada huo tatanishi ulipita kwa kura 315, huku kukiwa na wabunge 62 pekee walioupinga na wawili wakakosa kupiga kura.

Chini ya sheria za sasa, Rais Museveni, 73, hangeruhusiwa kuwania tena mamlaka hayo kwenye uchaguzi wa urais utakaokuwa mwaka wa 2021 kwani wagombeaji hawafai kuwa wenye umri wa zaidi ya miaka 75. Sheria hiyo mpya pia imerudisha kipengee kinachosema rais atakubaliwa kuwa mamlakani kwa vipindi viwili pekee.Kipengee hicho kilikuwa kimeondolewa wakati siasa ya vyama vingi ilipoanzishwa nchini humo mwaka wa 2005.

Sehemu hiyo ya sheria mpya itaanza kutekelezwa tu baada ya uchaguzi ujao, kumaanisha kwamba Museveni atakuwa huru kuongoza kwa awamu nyingine mbili.

Show More

Related Articles