HabariMilele FmSwahili

Shule ya Upili ya Pangani ndio iliyotia fora zaidi katika mtihani wa KCSE mwaka huu

Shule ya upili ya Pangani ndio iliotiwa fora zaidi katika mtihani wa KCSE mwaka huu. Waziri wa elimu Dr Fred Matiangi anasema mwanafunzi wa kwanza nchini anatoka katika shule hiyo mbali na kuwa shule hiyo imefanya vyema zaidi ikilinganishwa na miaka ya nyuma waziri Matiangi anasema kwa ujumla wanafunzi wa kike walifanya vyema zaidi katika mtihani wa KCSE mwaka huu wakilinganishwa na wenzao wa kiume Matiangi kadhalika anasema shule 10 hazitopokea matokeo yao ya KCSE kwani matokeo hayo yanadadisiwa kwa kina. Kulingana naye baadhi ya shule hizo zilijihusisha na visa vya udanganyifu akitoa mfano wa shule moja ambayo hatopokea matokeo yake, Matiangi anasema mwalimu mkuu wa shule hiyo alishirikiana na wanafunzi walioshiriki udanganyifu kuficha ushahidi.

Show More

Related Articles