People Daily

Wauzaji Mnazi Taita Taveta Wapewa Siku 30 Kusitisha Biashara Hiyo

Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja ametoa makataa ya siku 30 kwa wauzaji wa pombe ya kienyeji kusitisha biashara hiyo mara moja.

Kulingana na Samboja baadhi ya wenyejeji wa kaunti hiyo ni walevi kupindukia, jambo ambalo linalemaza maendeleo huku akiwataja machifu na manaibu wao kuchangia pakubwa kulemaza vita dhidi ya pombe haramu.

Kufuatia hayo kamishna wa kaunti hiyo Kula Hache ameapa kusaidiana na serikali ya kaunti kuhakikisha machifu na manaibu wao wanafanya majukumu yao

Show More

Related Articles