HabariMilele FmSwahili

Rais aagiza kuwafungulia mashtaka walimu walioshiriki udanganyifu katika mtihani wa KCSE

Jumla ya walimu 700 watafunguliwa mashitaka kwa tuhuma za kushiriki udanganyifu wakati wa mtihani wa KCSE mwaka huu. Rais Uhuru Kenyatta amemwagiza waziri wa elimu Dkt Fred Matiangi kwa ushirikiano na mkuu wa sheria pamoja na mkurugenzi wa mashitaka ya umma kuanzisha mchakato huo mara moja. Rais Kenyatta ametoa agizo hilo baada ya kukabidhiwa matokeo ya mtihani huo na waziri Matiangi. Rais aidha ameiagiza tume ya kuwaajiri walimu TSC kuwatuza walimu wakuu na wanaofunza masomo ambayo wanafunzi walifanya vyema zaidi. Pia kama sehemu ya utekelezwaji wa moja wapo ya ajenda kuu za utawala wake kwa muhula wa pili rais Kenyatta amemwagiza dkt Matiangi kuhakikisha wanafunzi wote milioni tatu wa shule za upili wanasajiliwa kwenye mpango wa hazina ya hospitali NHIF kuanzia januari mwakani.

Show More

Related Articles