HabariPilipili FmPilipili FM News

Watoto Na Walimu Wa Madrasa Wazuiliwa Na Polisi

Takriban watoto 100 na walimu 4 wa madrasa wanazuiliwa na polisi katika makao makuu ya polisi hapa mjini Mombasa baada ya kuokolewa na vikosi vya usalama.

Inadaiwa kuwa  watoto hao walikuwa wakishiriki masomo ya madrasa huko likoni kabla ya kutiwa nguvuni na maafisa wa upelelezi  hapo jana kwa madai kuwa wanahusishwa na ulanguzi wa watoto ikiwemo kupokea mafunzo ya kigaidi.

Inadaiwa kuwa jumla ya watoto 20 kati yao ni wa kutoka mataifa ya kigeni ikiwemo US, Britain, Canada, Afrika Kusini, Saudi Arabia, Somalia, Zambia na Uganda.

Mweka hazina mkuu wa Baraza la maimamu na wahubiri nchini CIPK Sheikh Hassan Omar amelaani kitendo hicho na kutaka watoto hao waachiliwe mara moja bila masharati yoyote.

Juhudi zetu za kutaka kuzungumza na maafisa wa usalama kuhusu suala hilo hazikufaulu.

Show More

Related Articles