HabariMilele FmSwahili

Jaji mkuu David Maraga awaidhinisha mawakili 53 kuanza kutekeleza majukumu yao rasmi

Jaji mkuu David Maraga amewaidhinisha mawakili 53 waliohitimu kuanza kutekeleza majukumu yao rasmi. Hata hivyo ameonya dhidi ya kujihusisha na visa vyovyote vya ukiuka wa sheria na utovu wa nidhamu. Anasema adhabu yake itakuwa kufutiliwa mbali kwa usajili wao na kupigwa marufuku kuhudumu kama mawakili. Maraga anasema lengo lao kuu ni kuhakikisha sheria inalindwa. Mawakili walioidhinishwa wameelezea ari yao ya kuanza kazi
Akiongea baada ya kuwapa zaidi ya wasomi 53 idhini ya kuhudumu kama mawakili nchini jaji mkuu David Maraga hakusita kuwaonya dhidi ya kutumia taaluma hiyo visivyo akisema adhabu yake itakuwa kali. Maraga amewakumbusha kuwa kiapo walichokula ni cha kuhakikisha sheria inalindwa.
Mawakili hao ambao sasa wataanza kufika kotini kuwatetea wateja wao wanasema wako tayari kwa kibaruia hicho baada ya kupata mafunzo .

Show More

Related Articles